JINSI YA KUFANYA MAKADIRIO YA GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA YAKO ANGALIA BAJETI YAKO KISHA TIZAMA MAHESABU HAYA YAFUATAYO. SEHEMU YA KWANZA: MAHESABU YA IDADI YA TOFALI ZINAZO HITAJIKA KWAAJILI YA UJENZI WA MSINGI NA KUTA (TOFALI ZA BLOCK). Habari wana Ujenzi!, nimegundua watu wengi wanapata changamoto ya kufahamu makadilio ya material wanayo hitaji katika ujenzi wa nyumba ama majengo mbalimbali. Kwasababu hiyo nimeamua kuanza mfululizo wa kutoa elimu hiyo na leo tutaanza na mahesabu ya idadi ya tofali zinazo hitajika kujenga Kabla haujaanza kufanya mahesabu lazima uwe na vitu vifuatavyo 1. Uwe na ramani yenye vipimo ili kujua ukubwa wa jengo lako. Ramani inachorwa na wasanifu majengo wataalamu ambao wanasomea — wataalamu hawa wanahitimu katika vyuo vinne tu hapa nchi navyo ni Ardhi University (chuo kikuu), na vyuo vya kati Ardhi Institute — Tabora, Ardhi Insitute — Morogoro, Institute of Lands Dar es Salaam. 2. Ufahamu aina ya material ama tofali utakazo tumia, kama ni hydraform, tofali...