Jinsi ya kupunguza uzito na kudumisha uzito huo mpya kwa muda mrefu

Kupunguza uzito ni lengo ambalo wengi wetu tunataka kufikia, lakini kudumisha uzito huo mpya kwa muda mrefu ni changamoto kubwa. Katika chapisho hili, nitazungumzia njia bora za kupunguza uzito na kudumisha uzito huo mpya kwa muda mrefu.

  1. Punguza kiasi cha chakula unachokula kidogo kidogo

BADALA YA KUJITESA KWA KULA MATUNDA NA MAJANI KILA SIKU. WEWE KULA CHAKULA UNACHOPENDA LAKINI:

a). kulingana na uzito unaotaka kupunguza (kama ni kwa kiasi kikubwa basi fanya hivi

- Pakua chakula unachopenda kama ni wali kuku maharage njegere etc kwenye sahani kwa kipimo unachokula kila siku. kisha GAWANYA CHAKULA HICHO MARA MBILI YANI NUSU KWA NUSU.

- Kula nusu moja tu na nusu nyingine mpatie mtu kabla hujaanza kula kabisa. Ama hifadhi kwa ajili ya mlo ufuatao Lunch HIFADHI kwa ajili ya dinner.

:- HII INAMAANISHA UMEPUNGUA MLO WAKO KUFIKIA NUSU YA CHAKULA UNACHOINGIZA MWILINI KILA SIKU.

b). Kula taratibu sana nusu hio ili uweze kufurahia kama ambavyo ungefurahia kikiwa kamili.

Kupunguza kiasi cha chakula unachokula kunaweza kukusaidia kupunguza uzito wako. Hata hivyo, badala ya kubadili chakula chako na kuanza kula matunda pekee, unaweza kudumisha lishe bora na kupunguza kiasi cha chakula unachokula kidogo kidogo ili kupunguza kalori. Punguza kalori zako polepole na kwa utaratibu, badala ya kujaribu kupunguza kalori kwa kasi sana.

2. Ongeza shughuli za kila siku

Mazoezi ni mazuri lakini ni nadra sana kupata motisha kama huna motisha basi Ongeza shughuli zako za kila siku hususanikutembea.

    a). Paki gari lako mbali na ofisi au mahala unapokwenda ili ulifuate ukitembea.

    b). Shukia kituo kimoja kabla ya kituo unachoshikia kila siku ili utembee kuelekea unapokwenda

    c). Pendelea kutembea tembeandani ya nyumba yako zunguka usikae tu muda wote.

Kuongeza shughuli za kila siku ni muhimu sana katika kupunguza uzito na kudumisha uzito huo mpya kwa muda mrefu. Badala ya kufanya mazoezi ambayo ni ngumu na hayawezi kudumishwa kwa muda mrefu, unaweza kuanza na shughuli ndogo na rahisi kama kutembea kidogo kila siku, na kuziongeza kidogo kidogo kila wiki ili kuongeza kiwango chako cha shughuli.

KWANINI NJIA HII NI BORA:

1. NI RAHISI

2. HAI HITAJI JITIHADA KUBWA

3. MATOKEO YAKE HUDUMU MUDA MREFU KWASABABU UNAKUWA UMEJENGA TABIA.


Mfano halisi KUSUDI UELEWE KINACHOFANYIKA KATIKA NJIA HII:

- Chukulia mwili wako kama stoo ya magunia ya mahindi. Yani unene wako ama kitambi chako na mafuta yaliyomo ni kama idadi ya magunia ya mahindi.

- Kila siku katika stoo hiyo unaweka magunia matatu mapya ya mahindi. na unatoa gunia moja.

yaani maana yake kila siku unakuwa umeongeza gunia jipya moja STOO BAADA YA KMWAKA ITAKUWA NA MAGUNIA MAPYA 365.

;-MAANA YAKE UTAONGEZEKA UNENE

SHUGHULI unazo fanya kila siku ni sawa na utumiaji wa magunia hayo.

sasa basi ukiwa unaweka kila siku nusu gunia ndani ya stoo yako hiyo mpya.


na kutoa magunia mawili. STOO YAKO ITAPUNGUA IDADI YA MAGUNIA.


CALORIES in simplex terms.


Basi fanya hivyo kwa miezi sita. Utaenjoy chakula ukipendacho na kupata matokeo ya kudumu.


ASANTE. KARIBUNI KWA MASWALI CHINI HAPA:

Comments